Nguvu ya Warumi duniani na athari za anguko la biblia takatifu.
Dola ya Rumi imeendelea kuwa mtawala wa ulimwengu kwa mambo mengi hasa ya kiroho. Utawala huu wa wakatoliki ndio ulioasisi imani za kiroho zote ulimwenguni na ndio ulioandika maandiko ya kiroho ambayo hutajwa kama maandiko yenye pumzi ya kiuungu, umekuwa ukiendelea kuamua mwenendo wa kiroho ulimwenguni na kuonekana katika dunia ya leo kama unaenda kinyume na kilichomo katika kitabu chao kitakatifu kiitwacho biblia, ambapo maranyingi biblia hii inakwenda na matakwa ya watafasiri na sio kilichoandikwa.
Wakati biblia inasisitiza katika Ufunuo wa Yohana 22:18-19 kuwa,
"Mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamuondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki".
Lakini utawala wa Ruma ulibadili matakwa hayo ya kibiblia katika nyanja nyingi za maisha ya binadamu, mfano ni Majira na Nyakati ya dunia. Wakati leo dunia inaaminishwa kuwa mwaka mmoja una siku 365, ukweli wa kiblia nikuwa mwaka mmoja una siku 336,
Wakati dunia ikiaminishwa kuwa mwezi una siku 28, 30 au 31, lakini ukweli wa kibiblia nikuwa mwezi mmoja una siku 28 tu. Dunia ikaaminishwa kwenye Januari ambalo ni jina la miungu ya warumi, lakini ukweli wa kibiblia ni kuwa mwezi wa kwanza huitwa ABIBU/NISANI, ukisoma Kutoka 12:2 au Kutoka 23:15 inafafanua vema maagizo ya Mwenyezi Mungu.
Ni kweli kuwa Kalenda tunayotumia leo hii ijulikanayo kama Gregorian Calendar iliamualiwa na Pope Gregory wa Roma mwaka wa 1585. Hata hivyo madabiliko makubwa yaliyofanywa na Papa Gregory ilikuwa ni kuondoa ongezeko la mwaka mmoja katika kila karne. Hii ilitokana na sababu kadhaa, ila moja kubwa ikiwa ni kufanya namba ya siku katika mwaka mmoja iendane sawa na namba ya siku zitumiwazo na dunia kuzunguka jua ikiwa hasa na lengo la kutaka kulipa jua dakika 11 na nusu zilizokuwa zinaongezwa na Julian Calendar kila mwaka.
Kwa muda mrefu sana kalenda za kirumi zilikuwa na miezi ama kumi, au kumi na mbili au kumi na tatu. Kalenda ya zamani sana ya kirumi ilikuwa na miezi kumi na siku 304 kama ifuatavyo:
Martius ( siku 31),
Aprilis (siku 30)
Maius ( siku 31)
Iunius ( siku 30)
Quintilis ( siku 31)
Sextilis ( siku 30)
Septimus ( siku 30)
Octo ( siku 31)
Novem ( siku 30)
Decemvis ( siku 30)
Ifahamike kuwa majina ya miezi minne ya kwanza yalitokana na majina ya miungu wa kirumi wa wakati huo:
Mungu wa vita (martius)- Mwezi huo baada ya baridi ndipo warumi walikuwa wakipigana vita.
Mungu wa mapenzi (Aprilis)- mwezi huo ndipo walikuwa wakijamiiana sana,
Mungu wa uzazi (Maius)- baada ya kuwa wamejamiiana sana mwezi Aprili, wanawake wengi walikuwa wakijifungua mwezi huu wa Maius,
Mungu wa ndoa (Janisu), mwezi huo ndipo vijana wengi walikuwa wakifunga ndoa.
Majina ya miezi sita inayofuata yalitokana na nafasi yake katika mwaka ambapo Quintlis ni namba tano ya kirumim Sextilis ni namba 6 septimus namba 7, Oto ni 8, Novem ni 9 na Decemvis ni 10.
Kutokana na elimu ya unajimu kuongezeka, kalenda hii ilikuwa ikifanyiwa mabadiliko kidogo kidogo ili iendane na unajimu. Mabadiliko hayo ni pamoja na kuingizwa kwa miezi mingine mitatu ya Ianuarius, Februarius, Mercedonius kabla ya Martius na hivyo kuhamisha mwezi Martius kutoka mwezi wa kwanza wa mwaka hadi kuwa mwezi wa nne wa mwaka. Jina Ianuaris lilikuwa na maana ya mlango wa kuanzia mwaka.
Mwaka 45BC, kalenda hii ilifanyiwa mabadiliko makubwa sana chini ya utawala wa Julius Caesar; mabadiliko haya yaliyoleta kalenda iliyojulikana kama Julian Calendar yalibadilisha idadi ya siku za mwaka kutoka siku 355 had siku 365 au 366 kama ifuatavyo hapa chini, na kuondolewa kwa mwezi wa Marcedonius.
Ianuarius (siku 31),
Februarius (siku 28 au 29)
Martius ( siku 31),
Aprilis (siku 30),
Maius ( siku 31),
Iunius ( siku 30),
Quintilis ( siku 31),
Sextilis ( siku 31),
Septimus ( siku 30),
Octo ( siku 31),
Novem ( siku 30),
Decemvis ( siku 31)
Baadaye majina ya miezi yaha yalikwenda kutoholewa na mataifa kuendana na lugha zao kama ilivyo kwa waswahili Januari, Aprili nk..
Lakini dhana kuu ya kiroho iko kinyume na waroma hawa, hivyo kutia shaka hata uinjilishi wa neno la Mungu kwa ujumla.
Sehemu nyingine ni kwenye uhalisia wa maadhimisho ya kuzaliwa masihi ama Yesu,
Kwa tafasiri ndogo nikuwa CHRISTMASS ni MUUNGANO Wa Maneno mawili yaani CHRIST & MASS,
Siku ya Tarehe 25 ADARI,
Hii Ilikua siku ya Kusherehekea MITAMBIKO YA KIPAGANI Kabla hata MWANA WA MUNGU, YESU KRISTO Hajaja Duniani, Baadae MWAKA WA 533AD, MTAKATIFU COSTANTINE, aliyekua Mkuu wa Kanisa La WARUMI (WAROMA ),ambalo siku hizi linajulokana kama KANISA,ROMAN KATOLIKI (Kanisa kongwe Zaidi Duniani).
Mtakatifu huyu aliibadili siku hiyo isiwe tena ya MITAMBIKO YA KIPAGANI BALI IWE SIKU YA KUMKUMBUKA MKOMBOZI, MWANA WA MUNGU YESU KRISTO, Na kuiita siku hiyo SIKU YA KUSANYIKO LA KRISTO YAANI CHRIST-MASS!
Maana ya CHRIST
Maama yake imetokana na neno la KIINGEREZA yaani (KRISTO),MESIAH, au MPAKWA MAFUTA, au ALIYETENGWA KWA KAZI MAALUMU.
Maana ya MASS
Hili limetokana na neno la
KIYUNANI,
Maana yake ni-KUSANYIKO, kwa hiyo maana ya neno
CHRIST-MASS ni KUSANYIKO la KRISTO.
Amini nawaambieni, historia yoyote huandikwa na mwenye nguvu. Udumu uishivyo na imani yako itakuponya.
Na Yericko Nyerere