Rais Wetu Aige Mfano wa Mwenzake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya....

Rais Wetu Aige Mfano wa Mwenzake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya....


Tumemsikia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipolihutubia Taifa lake baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya, kuwa anawaruhusu wafuasi wa mshindani wake mkuu kisiasa Raila Odinga kuwa wanaruhusiwa kuandamana na kuelezea hisia zao kwa kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba na akaliagiza Jeshi la Polisi la nchi hiyo liyalinde maandamano hayo na wala wasiwazuie wananchi hao kuandamana.Nimejaribu kulinganisha kauli ya Rais wa Kenya na kauli ya Rais wetu nimeona zinatofautiana sana kama umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!Tumeshuhudia hapa nchini kwetu Rais wetu akipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akijiruhusu yeye mwenyewe na chama chake kuendelea na shughuli za kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.Tumewahi kumsikia Rais wetu wakati ule ambapo vyama vya upinzani waliopokuwa wakipanga maandamano waliyoyapa jina la UKUTA, Rais wetu alipiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi!Tumeshuhudia nchini kwetu viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani wakikamatwa na Jeshi la Polisi hata pale wanapofanya vikao vya ndani kwa kile ambacho kimekuwa kikiitwa tuhuma za uchochezi kwa kile ambacho Jeshi hilo limekuwa likidai ni maelekezo toka juu.........Kama nchi yetu inaongozwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inaelezea kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vina Uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa, sasa ni kwa nini Rais wetu anaamua kuivunja Katiba ya nchi yetu na kuamua kuendesha nchi yetu iwe kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja?

 



Back To Top