Tume ya IEBC imesema kuwa hakuna udukuzi wowote uliofanyiwa mfumo wake wa kutoa matokeo ya uchaguzi kielektroniki.
Afisa mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema kuwa mfumo huo uko salama, Akivihutubia vyombo vya habari katika makao makuu ya IEBC katika eneo la Bomas jijini Nairobi, amesema kwamba mfumo huo haukuingiliwa kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi.
Amesema kuwa madai ya upinzani kwamba mfumo huo ulidukuliwa ili kumsaidia rais Uhuru Kenyatta kupata ushindi hayana msingi wowote.
Amesema kuwa maafisa wa tume hiyo waliufanyia uchunguzi mfumo huo hususan funguo zake na wakati kwamba hakuna tatizo lolote.

''Hakuna mtu aliyepewa funguo za kuingia katika mfumo huo hadi siku moja labla ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa kuna maadili',alisema Chiloba.
''Iwapo una ripoti zozote kuhusu vitisho vya mfumo wetu tushirikiane kwa sababu mfumo huu sio wetu bali ni wa raia wa Kenya'',aliongezea.Bw Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC.Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia, wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake.Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia.