Tetesi ...Serikali Kununua Ndege Mpya kwa Ajili ya Viongozi Wakuu wa Serikali....

Tetesi ...Serikali Kununua Ndege Mpya kwa Ajili ya Viongozi Wakuu wa Serikali....



Habari toka katika vyanzo vya uhakika vya hapa na pale vinaeleza kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kununua ndege mpya ya Rais yenye hadhi ya VIP,itakayo kuwa inatumika kwa usafiri wa ndani na nje ya nchi kati ya Rais,Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Ndege hiyo aina ya Falcon 2000LX toka kampuni ya Dessault Falcon Jet Corporation ni moja kati ya ndege za kisasa,zenye ubora wa hali ya juu na zinazotumika na watu maarufu na viongozi wa baadhi za nchi katika Afrika na Ulaya.

Falcon 2000LX ni ndege yenye uhitaji mdogo wa mafuta,kusafiri umbali mrefu bila kutua,yenye ubora wa kustahimili kutua katika viwanja vingi vya pembezoni mwa Tanzania na pia upatikanaji wa vipuri vyake ni rahisi.

Hii inaweza kuwa mbadala wa ndege ya Rais iliyonunuliwa enzi za Mstaafu Benjamin Mkapa na Mtunza fedha wake Basil Mramba.

Ndege hiyo ya "Watanzania wale nyasi" ni ndege yenye gharama,inayohitaji kiasi kikubwa cha matunzo.Upatikanaji wa vipuri vyake na uendeshaji wake ni changamoto.Hivyo ujio wa F2000LX inaweza kupunguza gharama ktk usafiri wa Rais.

Falcon 2000LX ina uwezo wa kubeba abiria kati ya 06 hadi 08,ina muundo wa VIP.

Kwenye tovuti mbalimbali za biashara ya ndege,inaionyesha ndege aina ya Falcon 2000LX yenye usajili wa F-HNOA kuonekana maeneo ya jiji la Nairobi kabla ya kufika Dsm.Safari yake ikiwa ni kufika kwa mteja wake ili aweze kuikagua na kujiridhisha na ubora wake.


Kwa habari zilizopenyezwa,zinathibitisha ndege hiyo kufika Dsm kati ya May 09-13 kwa ajili ya timu ya wataalamu kuikagua na kuona kama inafaa kwa matumizi ya Rais na viongozi wengine wa Kitaifa.

Katika Tovuti za uuzaji ndege duniani,ndege hiyo aina ya F2000LX ambayo "records" zake zinaonyesha kuwa ilikaa Dsm-Tanzania kwa siku zaidi ya mbili,kabla ya kuruka kwenda Znz na kurudi tena Dsm.Tovuti hiyo pia inaionyesha ndege hiyo hiyo yenye usajili wa F-HNOA kuwa ni moja ya ndege iliyopo sokoni,na inazunguka katika sehemu za nchi za Afrika ili kuweza kuwafikia wateja wake.

Hivyo licha ya kuwepo na habari za "kupenyezewa",lakini bado ushahidi wa kimtandao unathibitisha kuwa ndege hiyo ipo "Sokoni" na wakati wowote itauzwa kwa mteja atakayefikia makubaliano na kampuni husika.

Kama Serikali ya Tanzania itakuwa imeamua kufunga "deal" na kampuni ya Dessault,ni wazi sasa serikali,kupitia Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA)wataenda kumiliki ndege aina ya Falcon2000LX.

Mpaka sasa,Wakala wa Serikali (TANZANIA GVT FLIGHT AGENCY) anamiliki ndege zaidi ya sita ikiwemo zile bombadia zilizokodishwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).Hivyo ujio wa F2000LX itafanya TGFA kuwa na ndege zaidi ya sita.

Ikumbukwe kuwa usafiri wa ndege kwa Rais ni jambo la muhimu na lazima,juhudi za Rais wetu kwa sasa ni kuhakikisha anaachana na ndege zenye mahitaji makubwa ya uendeshaji na kumiliki zile zenye kubana matumizi kuendana na dhana ya serikali ya kupunguza "anasa".Bila shaka bajeti ya ununuzi huu itatoka katika "mfuko" wa bajeti ya Ikulu na hivyo kupunguza kelele za hapa na pale.

 



Back To Top