VIDONDA vya tumbo ni mojawapo ya ishara za mwili kuanza kuishiwa maji, ni uharibifu wa kuta za ndani ya tumbo. Kwa maneno mengine, ni majeraha ndani ya tumbo.
Kwanini vidonda vya tumbo ni ishara ya mwili kuishiwa maji?
Asilimia 94 ya damu ni maji, ubongo wetu una zaidi ya asilimia 85 za maji, na tishu zetu laini zina asilimia 75 ya maji.Tunatumia maji kupumua nje, kila masaa 24 tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu nje.
Kwa sehemu kubwa miili yetu huishiwa maji kutokana na sisi kusubiri kiu ndipo tunywe maji. Ndiyo, haupaswi kusubiri kiu ndipo unywe maji, kiu ni ishara iliyochelewa ya mwili kuhitaji maji.
Akili ya kawaida inaniambia nikiwa na bustani ya mboga mboga au hata maua nitakuwa nikiimwagilia maji mapema asubuhi au jioni wakati jua tayari limezama na si mchana wakati wa jua kali, kadharika maji yakiisha ghafla kwenye injini ya gari ndani ya mwendo mrefu siwezi nikashuka tu kwenye gari na kuongeza maji kwenye injini!, ni lazima nisubiri injini ya gari ipowe ndipo niongeze maji mengine.
Tuendelee na vidonda vya tumbo …
Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH yaani potential hydrogen. Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.
Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate yako au ya mkojo wako kila mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye alkalini katika mwili wako ibaki kuwa ya 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.
Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.
Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini yaani matunda na mboga za majani na kunywa vinywaji vyenye asidi chache na ikibidi basi atumie vinywaji vyenye alkalini nyingi kama juisi ya limau, juisi ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.
Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo.
Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja katika kila watu wanne anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Dalili za vidonda vya tumbo
Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni kuchoka choka sana bila sababu maalum, kuuma mgongo au kiuno, kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia, kizunguzungu, kukosa usingizi, usingizi wa mara kwa mara. Maumivu makali sehemu ya mwili, kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali.
Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali. Dalili zingine ni kichefuchefu, kiungulia, tumbo kujaa gesi, tumbo kuwaka moto, maumivu makali sehemu kilipo kidonda, kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi.
Kutapika nyongo, kutapika damu au kuharisha, sehemu za mwili kupata ganzi n.k. Pia dalili zingine ni kukosa hamu ya kula, kula kupita kiasi, kusahahu sahau na hasira. Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.
Vidonda vya tumbo husababishwa na nini?
Linapokuja suala la nini husababisha vidonda vya tumbo unaweza ukapata stori nyingi bila idadi, lakini kwa kifupi kabisa; vidonda vya tumbo ni ishara za mwili kupungukiwa maji na kama matokeo ya asidi kuzidi mwilini kuliko alkaline. Vinaweza pia kuletwa na bakteria ajulikanaye kama H.Pyroli.
Vitu vifuatavyo vinahusika katika kuleta vidonda vya tumbo mwilini:
1. Asidi iliyozidi mwilini:
Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIDONDA VYA TUMBO.
Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi.
Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili. Kwanza, vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa, baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, n.k.
2. Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha:
Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.
Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo kama matokeo ya mfadhaiko na hakuna chakula cha kufanyiwa kazi au kumeng’enywa humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.
Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha kuwa akili hutumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50. !
Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.
Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili au mawazo yatokanayo na shida za maisha.
Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, watu waliopewa talaka na wale wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.
Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui. Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya mapigano au makabiliano na adui.
Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe tayari zaidi kwa mapigano, na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni inayohusika na uzalishwaji wa nguvu mwilini huongezeka.
Kadiri mfadhaiko unavyokuwa ni wa muda mfupi, ndivyo pia athari zake zinavyokuwa ni fupi. Lakini pindi mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo mengi kila mara, athari zake nazo hudumu kwa muda mrefu.
Dalili za mtu mwenye mfadhaiko
Ikiwa bila ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko. Dalili hizo ni:
1. Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote,
2. kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi,
3. kupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa
4. Kupoteza hamu ya chakula
5. Kukosa usingizi
6. Wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia kwa ujumla
7. Kupoteza kumbukumbu au hali ya kusahausahau na kushindwa kuamua
8. Kughadhibishwa na vitu vidogo, yaani mtu kitu kidogo tu ameshachukia
9. Kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu.
3. Sababu ya tatu inayosababisha vidonda vya tumbo ni Haraka haraka
Maisha ya kisasa yanataka haraka katika kazi nyingi tuzifanyazo kila siku, ni lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo. Mbanano wa ratiba katika shughuli zako za kila siku pia husababisha matumbo nayo kubanana.
Malalamishi makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: “Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo, au nasikia kiungulia baada ya kula”. Haraka haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya matatizo haya.
Tumbo ni kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia hufungia breki kwenye viungo vya ndani. Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli na hapo husababisha kiungulia na maumivu.
Ili kuepuka kufanya kazi zako kwa hali ya uharakaharaka unashauriwa kupanga kabla ni kazi gani na gani utaenda kuzifanya siku inayofuatia kwa kuziandika kabisa katika karatasi au kitabu maalumu kiitwacho kiingereza diary au kumbukumbu za kila siku kwa Kiswahili na mhimu ni uwe na kiasi kwa kila jambo kwani si lazima umalize kazi zote leo.
4. Sababu ya nne ya kutokea vidonda vya tumbo ni ulaji wa Vyakula vya kusisimua
Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile ketchup, chill sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni. Sababu ni kuwa, visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo.
5. Vinywaji na vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi
Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi kama vile chai ya rangi, kahawa, soya sauce, mayonnaise, jibini, Vyakula jamii ya Mkate, samaki wa kwenye makopo, pombe, soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.
Utambuzi wa vidonda vya tumbo
Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni. Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.
MAMBO YA MHIMU YA KUZINGATIA ILI UPONE VIDONDA VYA TUMBO:
Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.
Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.
Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.
Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu. Pia unashauriwa kufanya yafuatayo katika kujitibu au kujikinga na vidonda vya tumbo:
Moja; Punguza haidrokloriki asidi:
Kama tulivyoona kule mwanzoni kuwa moja ya sababu ya kutokea kwa vidonda vya tumbo mwilini ni uzarishwaji wa haidrokloriki asidi ambayo huzalishwa tumboni dakika chache kabla hujaanza kula chakula ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. HAIDROKLORIKI ASIDI hii ni lazima ipunguzwe makali (must be neutralized) kabla hujameza chakula.
INAPUNGUZWAJE MAKALI? kwa kunywa maji kikombe kimoja au viwili nusu saa kabla ya kula chakula. Kwahiyo kama umepanga kuwa saa saba kamili mchana ndiyo utakula chakula cha mchana, basi saa sita na nusu unywe maji vikombe viwili. Kwa kufanya hivi kila mara kabla ya kula basi hakuna vidonda vya tumbo utakavyovipata kama matokeo ya hii haidrokloriki asidi.
Mbili; Pata usingizi wa kutosha:
Ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika zama zetu hizi. Haraka na pilikapilika za dunia yetu ya kisasa hazina mfano. Mvurugiko wa mawazo kutokana na mwenendo wa maisha uko kila mahali. Kutokana na mahitaji ya maisha, kuna idadi kubwa ya watu ambao neva zao hazitulii.
Kulala ni moja ya tiba za mwili. Usingizi husaga chakula na huondoa uvimbe katika tumbo, udhaifu na uchovu.
Kukesha usiku kucha husababisha kutosagika kwa chakula tumboni na hudhoofisha akili na pia husababisha akili kuvurugika. Kulala huleta pumziko kamilifu la mwili na akili.
Madaktari wetu wanasema kuwa, kulala ni muda ambao metaboliki ya mwili hufanyika polepole kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya makuzi ya afya njema ya mwili na akili.
Sehemu ya kulala inatakiwa iwe ni tulivu na isiyo na kelele, pia iwe na hewa safi na asilia. Hewa asilia ina athari nzuri katika mwili wa mwanadamu, miongoni mwa athari zake ni kuiwezesha akili kufanya kazi barabara, na pia huongeza hamu ya kula.
Kiwango cha wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri. Katika umri wa miaka miwili, mtu hushauriwa kulala masaa 14 hadi 16 kwa siku. Miaka minne masaa 12 hadi 14 kwa siku, miaka sita hadi minane masaa 11 hadi 12 kwa siku, miaka minane hadi 11 masaa 10 hadi 11 kwa siku, miaka 14 hadi 18 masaa 8 hadi 9 kwa siku. Watu wazima wanahitaji saa za kulala kati ya sita na nane kwa siku.
Tatu; Dhibiti mfadhaiko:
Mbinu ya tatu katika kujikinga na kujitibu vidonda vya tumbo ni kujitahidi kwa kila namna kudhibiti mfadhaiko. Tambuwa kuwa kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara. Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza kusababisha maradhi kama vidonda vya tumbo, maradhi ya moyo, n.k.
Mfadhaiko unaweza kuwa wa muda au wa kudumu. Matokeo yake yana madhara makubwa kama hautadhibitiwa. Ni vipi unaweza kudhibiti mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha? Unachotakiwa kufanya ili kujidhibiti na mfadhaiko wa namna hii ni kuridhika na maisha.
Kama utakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, ukaacha kuyakopa maisha ya jana na ukaacha kuhofu maisha ya kesho, ni hakika kabisa tumbo lako pia litatulia.
Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara wote duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo. Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.
Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa hisia una matokeo chanya katika mwili, pia wasiwasi na hofu ya maisha huweza kuleta magonjwa yanayoweza kuuwa kabisa sawa sawa kama inavyotokea pia kwa magonjwa yale yatokanayo na lishe dhaifu. Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.
Nne; Punguza au acha kabisa vinywaji na vyakula vifuatavyo:
Chai ya rangi, kahawa, pombe, soda, juisi za viwandani, sigara na tumbaku zote mpaka hapo utakapopona. Kama wewe ni mpenzi wa kunywa chai asubuhi au jioni basi sijasema usinywe chai, bali unachotakiwa kufanya ni kuchemsha maji yako ya chai na uiunge na ama tangawizi, mdalasini, au mchaimchai na uendelee na chai yako, kinachoepukwa hapa ni yale majani meusi ya chai ambayo ndani yake huwa na kaffeina na asidi nyingi na hivyo kuwa chanzo cha vidonda vya tumbo. Lakini pia tambuwa kuwa tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini, hivyo unapokunywa chai ya tangawizi faida nyingine unayopata zaidi ya kuondoa njaa au kushiba ni dawa iliyomo ndani yake, hivyo unashiba huku unajitibu, unaionaje hii siyo imetulia?.
DAWA MBADALA 9 ZINAZOTIBU VIDONDA VYA TUMBO:
Chagua dawa 3 kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri haraka zaidi. Sasa usinywe zote wakati mmoja, moja tumia asubuhi, nyingine mchana na nyingine jioni. Kumbuka usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari.
1. UNGA WA MAJANI YA MLONGE
Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.
Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi au unaweza kuuchanganya kwenye chakula kama vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo.
2. KABEJI
Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.
Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.
*Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.
*Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.
*Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.
3. NDIZI
Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.
Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.
Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.
Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.
4. NAZI
Nazi ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. Nazi huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la nazi na maji ya nazi (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.
Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la nazi au maji ya nazi kila siku. Pia unaweza kuitafuana nazi yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.
Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi.
5. UWATU
Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwakuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika kama utando na hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.
Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.
Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.
Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.
Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa kama vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona.
6. ASALI MBICHI
Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. Kama ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.
Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.
7. KITUNGUU SWAUMU
Kitunguu swaumu pia husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center in Seattle waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu swaumu unacho katika kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini unaweza kudhiti pia bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo ajulikanaye kama Helicobacter Pylori (H. pylori).
Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara 1 kwa wiki 2 au 3
8. MKAA WA KIFUU CHA NAZI
Mkaa pia hutibu vidonda vya tumbo hasa mkaa utokanao na vifuu vya nazi. Chukua vifuu vya nazi vitano au kumi vilivyokauka, viweke juu ya jiko la mkaa au popote na uvichome moto, mwishoni chukua mkaa wake usage kupata unga, kisha chota kijiko kikubwa kimoja na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji changanya vizuri na unywe kutwa mara 3 kwa wiki 2 au 3.
9. MAFUTA YA HABBAT SODA
Ni moja ya dawa za asili chache zinazoweza kutibu vidonda vya tumbo moja kwa moja. Tafiti nyingi zinathibitisha mafuta ya habbat soda yanatibu aina zote za vidonda vya tumbo!
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hadi siku 60 hasa habbat soda grade 1. Vidonda vya tumbo pia upate unga wa asili wa majani ya mlonge na mbegu za maboga kwa matokeo mazuri na ya uhakika, kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha kila siku, epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.
Umewahi kuwa na vidonda vya tumbo kabla na ukapona? tusaidie ni dawa gani ulitumia ili tusaidie na wengine wanaoendelea kuteseka bila sababu.
Ikiwa utahitaji dozi kamili ya dawa za asili zilizoandaliwa tayari kwa ajili ya vidonda vya tumbo niachie ujumbe WhatsApp +255769142586, natuma pia kwa walioko mikoani.
Ofisi yangu inaitwa Victoria Home Remedy ipo Buza Sigara temeke unaingia kupitia jet corner (uwanja wa ndege) au tandika.
Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya uwapendao