Mtoto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka tisa ambaye anaishi na virusi vya UKIMWI toka azaliwe nchini Afrika Kusini ameishi kwa muda wote huo bila kunywa dawa ya kupunguza makali ya ugonjwa huo baada ya kupatiwa matibabu muda mfupi baada ya kuzaliwa – miaka tisa iliyopita, wamesema madaktari nchini humo.
Mtoto huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa kulinda taarifa zake, alipatiwa matibabu makubwa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Ameweza kuishi bila kuonesha dalili za maradhi hayo kumzidi tangu alipoachishwa matibabu miaka nane-na-nusu iliyopita.
Ndugu na wanafamilia wa mtoto huyo wamesema wana furaha kwakuwa watu wengi wanahitaji matibabu ya kila siku kudhibiti virusi vya UKIMWI visishambulie mfumo wa mwili kujilinda dhidi ya maradhi.
Madaktari wanasema kuwa kuelewa nini kilichosababisha mtoto huyo aweze kuishi salama kwa miaka yote hiyo kunaweza kusababisha kupatikana kwa chanjo dhidi ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI.
Mtoto huyo alipata maambukizi kutoka kwa mama yake wakati anazaliwa mwaka 2007 na kipindi hicho kipimo kilionesha kuwa na kiwango kikubwa cha virusi vya UKIMWI kwenye damu yake.
Matumizi ya dawa zaidi ya mbili za kupunguza makali ya virusi hivyo kwa wakati mmoja haikuwa ni jambo lililozoeleka kwa wakati anazaliwa lakini mtoto huyo aliweza kuanzishwa tiba hiyo tangu akiwa na umri wa wiki tisa kama jaribio la tiba ya aina hiyo kwa binadamu baada ya wazazi wake kukubali mtoto wao kufanyiwa majaribio ya tiba hiyo.
Virusi vya ugonjwa huo vilitoweka hivyo madaktari kuamua kusitisha dozi baada ya wiki 40 toka aanze kutumia, na tofauti na kwa watu wengine waliojumuishwa kwenye jaribio hilo – kwake virusi hivyo havijarudi mpaka sasa.
Matibabu hayo yanayoanzishwa muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa mtoto yanalenga kushambulia virusi kabla havijapata nafasi ya kukomaa vizuri yamekuwa yakitumika kwenye tiba ya mtoto mara mbili tu kabla ya hapo.
Mtoto mmoja mjini Mississippi “Mississippi Baby” alipatiwa tiba ya aina hiyo ndani ya saa 30 tangu azaliwe na akaishi kwa miezi 27 bila matibabu yoyotekabla ya virusi hivyo kurudi tena kwenye damu yake.
Mtoto wa pili aliyepatiwa matibabu ya aina hii ilikuwa ni nchini Ufaransa kwa mtoto ambaye mpaka sasa ameishi kwa miaka 11 bila kutumia dawa zozote.
Mkuu wa Utafiti wa Magonjwa kwa watoto katika kituo cha utafiti cha Perinal jijini Johannesburg, Dkt. Avy Violari amesema: “Hatuamini kwamba tiba hii ya kuchanganya dawa zaidi ya moja pekee inapelekea virusi kuisha.
“Kwakweli mpaka sasa hatuijui ni kwa sababu gani mtoto huyu amefikia hatua hii ya virusi kutoweka – tunaamini sababu yaweza kuhusiana na tabia za kimaumbile au mfumo wa mwili wake wa kujilinda dhidi ya magonjwa.”
Kuweza kugundua, kukijumuisha kwenye matibabu mapya ya ugonjwa huu – kama chanjo au tiba – kutaongeza nafasi ya kusaidia wagonjwa wengine.
Ni muhimu kujua kuwa ingawa hakuna virusi hai vya UKIMWI mwilini mwa mtoto huyo, virusi hivyo vimeendelea kuwepo kwenye mfumo wake wa kinga ya mwili.
Virusi vya UKIMWI vina uwezo wa kujificha humo – kitaalamu hujulikana kama (latent HIV) – kwa muda mrefu sana, kwahiyo, bado kuna uwezekano kuwa mtoto huyo anaweza kuja kuhitaji tiba katika miaka ya baadae.
Profesa Diana Gibb wa nchini Uingereza aliliambia Shirika la Utangazaji la BBC kwamba: “Inatia moyo sana kwa sababu unaona mfano wa chanjo tunayoitafuta kwahiyo inatia hamasa kuona matokeo kama haya.
“Lakini ni muhimu kujua kwamba haya ni matokeo ya mtoto mmoja tu. UKIMWI bado ni tatizo kubwa ulimwenguni na hatutakiwi kuelekeza macho yetu yote kwa mtu mmoja tu kama hivi badala ya kuliangalia tatizo hili kwa ukubwa wake uliopo barani Afrika.”

Uwezekano wa kinga
Baadhi ya watu wana uwezo mkubwa wa kiasili wa mwili kudhibiti virusi vya UKIMWI lakini chochote ambacho mtoto huyo atakuwa nacho mwilini mwake ni tofauti kabisa ambacho hakijawahi kuonekana kwa binadamu.Kuweza kugundua, kukijumuisha kwenye matibabu mapya ya ugonjwa huu – kama chanjo au tiba – kutaongeza nafasi ya kusaidia wagonjwa wengine.