Leo Katika Historia- Septemba 9 1990: Kifo cha Dikteta Samuel Doe wa LIBERIA...!

Leo Katika Historia- Septemba 9 1990: Kifo cha Dikteta Samuel Doe wa LIBERIA...!


Samuel Kanyon Doe alizaliwa May 6, 1951 jijini Tuzon, nchini Liberia.

Alfajiri ya 12 Aprili 1980, kikundi kidogo cha wanajeshi 17 kilijipenyeza ndani ya makazi ya Rais jijini Monrovia... Ikulu walimkuta Rais William Tolbert bado amelala wakamuua.

Aliyeongoza kikundi hicho alikuwa askari kijana na wa cheo cha chini, Sajenti Samuel Doe.

Inasemwa kuwa Doe alipoingia Ikulu na
wenzake, alidhani watakwenda kumlalamikia Rais juu ya mishahara midogo ya askari wa vyeo vya chini.

Lakini jinsi walivyoikuta Ikulu
ikiwa nyepesi vile, ndivyo mipango ilipobadilika na kuamua kumuua Rais mwenyewe na kuchukua madaraka.

Samuel Doe alikuwa askari ambaye hata
madarasa manne ya shule ya msingi
hakuyamaliza alitoka kabila dogo la waishio misituni, kabila la Krahn.

 Watu wa kabila kama lake, masikini na ambao ndio waliotoka vijijini na kukimbilia jijini Monrovia kutafuta vibarua na pesa.

Kwa wenye bahati, kama Samuel Doe, walionekana mitaani na kuitwa
kujiunga na Jeshi.

Na kama ilivyokuwa kwa Idi Amin, Urais
ulimdondokea tu Samuel Doe, kama vile mtu aliyeshinda bahati nasibu.

Ujio wa Samuel Doe uliwafaya WaLiberia
waamini kuwepo kwa mabadiliko
Kuondokana na utawala wa kifisadi na
kirasimu wa William Tolbert.

Samuel Doe akajitangaza kuwa Rais, April 12,v1980... Haraka sana akawatwanga risasi mawaziri wote wa Tollbert katika Pwani ya Nchi hiyo  huku wananchi wakitazama kama mechi ya mpira.

Sajenti Samuel Doe akatawala kwa kipindi cha miaka kumi Nchi ikawa kama imesimam watu wa kabila la Samuel Doe waliogopewa na makabila mengine  waliweza kufanya lolote lile na hakuna aliyewagusa

Waliua na waliwatisha wengine wengi wasio wa kabila la Rais Doe waliishi kwa hofu kubwa kile ambacho kila mtu asiye wa kabila la Doe, alikuwa anakisubiri kushuhudia mwisho wa Sajenti Samuel Doe.

Anatokea Charles Taylor huyu alikuwa rafiki wa zamani wa Sajenti Samuel Doe Lakini, urafiki wao ulikufa pale Samuel Doe
alipodai kuwa Charles Taylor alimtapeli dola milioni moja.

Kisha Taylor akatorokea Marekani,Huko akaanza kufanya biashara kwa mtaji wa fedha alizomtapeli Sajenti Samuel
Doe Charles Taylor naye akaishia gerezani nchini Marekani kwa mashtaka ya utapeli Lakini akatoroka jela na kukimbilia Ivory Coast.

Akiwa Ivory Coast, Charles Taylor akaanza
kujipanga kwenda kuuangusha utawala wa
Sajenti Samuel Doe… Charles Taylor akiwa
alikiandaa kikosi cha wapiganaji 60.

Kikosi kilikuwa tayari kwa kuingia
Monrovia kumwondoa Samuel Doe
madarakani ilikuwa ni mwaka 1989.

Wakati huo, wajuzi wa masuala ya kijeshi waliamini kabisa, kuwa Sajenti Samuel Doe angeweza, kirahisi kabisa, kumteketeza kijeshi Charles Taylor na kikosi chake cha watu 60.

Sajenti Samuel Doe angeweza kufanya hivyo hata kabla Charles Taylor hajavikaribia viunga vya Monrovia
Badala yake, ‘’Master Sergeant’’ Samuel Doe, aliwatuma mstari wa mbele, wanajeshi kutoka kabila lake la Krahn... Ni wanajeshi wa kuokoteza ambao wengine hawakuwa hata naviatu.

Wanajeshi wale wa Samuel Doe, njiani
wakitokea mji mkuu Monrovia wakielekea
uwanja wa mapambano, wakaanza kufanya
wizi wa Pesa,Vitu vya dhamani na mali za watu.

Habari za askari ‘’vibaka’’ wa Samuel Doe
zikasambaa haraka kwenye vijiji vya msituni huko watu wakajitolea kujiunga na vikosi vya Charles Taylor kukabiliana na askari wa Samuel Doe.

Jeshi la Taylor likakua kwa haraka… Baada ya miezi sita tu, likaingia kwenye viunga vya mji mkuu wa Liberia, Monrovia, June 1990.

Ndipo hapo kwenye kambi ya Charles Taylor ugomvi ukazuka… Nani atakuwa Rais
Nani atakuwa na mamlaka ya hazina kuu.

Ni ugomvi uliowatenganisha Charles Taylor na Prince Johnson aliyeamua kuachana na Taylor na yeye kuanzisha kikosi chake.

Wote wawili walikuwa na tamaa ya Ikulu. Vita sasa ikawa ya vikosi vitatu kugombania kuingia Ikulu ya Monrovia: Kikosi cha Sajenti Samuel Doe kinachojihami, kikosi cha Charles
Taylor na kikosi cha Prince Johnson.

Wote wakaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe kugombania Ikulu ya Monrovia.
Mitaa ya Monrovia wakaonekana askari wa
makundi tofauti wakipigana. Hata watoto
waliingizwa kwenye vita vile vya
kiwendawazimu.

Hatimaye, mwishoni mwa mwezi August 1990,vikosi kutoka nje viliingilia mgogoro ule.

Vikosi vya Nigeria chini ya mwavuli wa
ECOMOG, ni umoja wa mataifa ya Afrika
Magharibi… Ecomog walikuwa na jeshi
lilioongozwa na kamanda kutoka Nigeria...
Jeshi hilo lilifika Monrovia na meli kubwa ya kijeshi.

Jumapili Septemba 9, 1990, Rais Samuel Doe aliposikia habari za ujio wa ECOMOG, akafanya kosa kubwa la kuamua kutoka Ikulu na kwenda mwenyewe bandarini kuonana na kamanda wa vikosi hivyo vya majeshi ya Nigeria.

Samuel Doe hakuwa na msafara
mkubwa... Aliwachukua walinzi wake na
kuingia kwenye Mercedes Benz kuelekea
bandarini.

Masikini, Rais wa nchi akajikuta anapita
kwenye mji wenye miba… Akafika bandarini na hapo Prince Johnson alikuwa amewapanga askari wake kumshughulikia Samuel Doe.

Zikapigwa risasi na walinzi wote wa Samuel Doe wakapoteza maisha Samuel Doe mwenyewe risasi ilimpata mguuni na hakuweza kukimbia, akakamatwa.

Akafungwa kitambaa usoni na akapelekwa
kwenye kuteswa... Prince Johnson
akahakikisha mateso yale yanarekodiwa kwa Camera za filamu kwenye filamu hiyo, Prince Johnson anaonekana akipungiwa upepo na mwanadada huku akinywa bia na kumwangalia rafiki yake wa zamani, Samuel Doe akiteswa.

Muda mwingi Prince Johnson alikuwa akimtaka Samuel Doe aseme zilipo fedha kwenye hazina.

Kuna wakati alisikika Samuel Doe akimwita
rafiki yake wa zamani kwa jina alilozoea
kumwita: "Prince, waambie walegeze kamba walizonifunga, nitasema kila kitu, walegeze hizo kamba kwanza!"

Ukweli, kamba walizomfunga kwenye miguu na mikono zilikaza sana na kumletea maumivu makali.

Waliendelea kumpiga huku wakimtaka ataje ilipo hazina. Walimtaka ataje akaunti yake ya benki.

Ndivyo ilivyokuwa barani kwetu Afrika, na labda mpaka leo… Rais dikteta anapopinduliwa, kikubwa kinachotafutwa ni namba ya akaunti ya benki alikoficha fedha

Mara nyingi ni kwenye benki za nje… Ndio, inahusu hazina ya nchi "Mkateni sikio kama hataki kusema!" Alisikika
Prince Johnson akitamka kwa hasira.

Askari wale wakamtupa Samuel Doe sakafuni, wakamkata sikio moja…
"Mkateni sikio lingine!", alisikika tena Prince Johnson akitamka.

Baada ya hapo, Rais Doe aliuawa kikatili
Jumapili hiyo jioni, Septemba 9, 1990 baada ya kukatwa masikio yake, sehemu zake za siri na baadhi ya vidole vya miguu na mikono na hatimae mwili wake ulitembezwa mitaa Mbalimbali ya jiji la Monrovia…

Huo ndio ulikuwa mwisho wa Dikteta Samuel Kanyon Doe wa Liberia.

Baada ya mauwaji hayo Prince Johnson
Testimony akajitangaza kuwa rais wa Liberia lakini hakudumu alikimbilia Nigeria baada ya kuzidiwa na wapiganaji wa Charles Taylor.

Huko Nigeria akaokoka akamtumikia mungu kanisani, na kuiomba radhi familia ya Doe.

Mnamo mwaka 2004 Prince alirudi
Monrovia.

           _*```MWISHO```*_
 



Back To Top